Mix

Seneta wa Nairobi Mike Sonko ‘sharobaro’ ameamua kuonyesha mshahara anaolipwa na matumizi yake.

on

sonkoUnaambiwa Seneta wa Nairobi Mike Sonko maarufu kama mbunge Sharobaro time hizo, amepost payslip yake kwenye Facebook ikionyesha mshahara anaochukua na matumizi yake kwa mwezi March.

Mike Sonko anakua kiongozi wa kwanza nchini Kenya kuweka wazi kiasi cha pesa anachopokea kama mshahara na matumizi yake ambapo kwa mujibu wa jarida la NN au Nairobi News Payslip hiyo inaonyesha seneta Sonko anapokea mshahara wa shilingi 532,705 pesa za Kenya kila mwezi.

TZA SENETA MIKE SONKO NA PAYSLIP YAKESeneta Sonko anadai kwamba pesa anayopokea hupeleka kanisani kama sadaka na mchango wake wakati wa hafla ya michango au Harambee.

Miongoni mwa matozo katika mshahara wake ni ya kulipa mkopo aliouchukua kutoka kwa benki ilikuwasaidia waathirika wa mkasa wa moto wa Sinai [mwaka wa 2011 alipokua mbunge wa Makadara] kufanyiwa upasuaji na kukimu ada ya hospitali.

Hii ndio list ya makanisa yanayopata pesa kutoka kwenye mshahara wa Sonko mwezi machi 2014.

 • Nairobi calvary temple Buruburu Ksh 50,000
 • Pentecostal church eastleigh (kiambio) Ksh 50,000
 • AIC Jericho Ksh 100,000
 • PCEA bahati Ksh 100,000
 • PCEA Kangemi Ksh 30,000
 • FPFK Church Kibera Ksh 30,000
 • Kawangware Methodist Ksh 30,000
 • PCEA Lunga Lunga Ksh 30,000
 • St. Francis Assis Mombasa Ksh 30,000
 • Sister Vivenzia memorial foundation Ksh 50,000
 • PCEA Umoja Ksh 30,000
 • PCEA Kangemi Ksh 30,000
 • Jesus winners ministry Roysambu Ksh 30,000
 • Makongeni SDA Kshs 40,000
 • St. Joseph Catholic Church Mumbi Muranga Ksh 200,000
 • AIC Yakamete Ngelani Ksh 100,000
 • Free Medical Camp in Deep Sea Slum Ksh 450,000
 • Teen Challenge Kenya rehab center Ksh 200,000

 

Tupia Comments