beef

Majibizano kati ya Soundcity TV na manager wa P Square yanaendelea… hili ndio tamko la Soundcity!!

on

Beef la Soundcity TV na P Square ikiwemo manager wao Jude Okoye bado linaendelea na pengine litaendelea kwa muda mrefu.

Soundcity TV imekerekwa na kauli ya manager wa P Square Jude Okoye iliyosema kuwa; “nyinyi mnapata mamilioni ya pesa lakini wasanii hawalipwi fungu lao kwenye hayo mamilioni”…  kwa hasira wamepost picha inayoonyesha kama kumshushia heshima manager wa P Square na kuandika ujumbe mrefu sana kujibu tuhuma hizo…

SOUND2

 

Cha kwanza ambacho Soundcity TV imesema ni kwamba wanatambua kuwa hawawapi P Square favour yoyote kwani wakiwa na kazi nzuri na wakiileta kwenye kituo hicho, Soundcity haitakiwi kuikataa bali kuipromote kazi hiyo kwenye platform mbalimbali walizonazo kwani kusupport kazi za wasanii sio ombi la msanii bali ni jukumu lao.

Kuhusu kutokulipa wasanii fungu lao Soundcity TV wamekataa kabisa kitendo hiki na wamesisitiza kuwa kazi ya manager ni kupokea na kuthibitisha kuwa amepokea ile asilimia yake na ya msanii iliyotokana na wimbo wao kupigwa kwenye kituo hicho cha TV…

SOUND

>>>“Kazi yako kama manager ni kuhakikisha wasanii wako wanapata mafungu yao kutokana na kazi zao kuchezwa kwenye TV, ukifuatilia kupitia COSON, MSCN utagundua kuwa SOUNDCITY inawalipa wasanii mafungu yao kila mwaka… COSON ni Chama cha Haki Miliki Nigeria na MSCN ni Chama cha Haki Miliki na Muziki Nigeria, pengine ungeweza kujifunza zaidi kuhusu hivi vitu viwili kupita tovuti yao http://www.cosonng.com… <<< SOUNDCITY.

Soundcity Tv wameendelea kusema…

sound3

>>> “Mnasema mna haki ya kuchagua kama mnataka kufanya kazi na brand yetu au la na mmechagua kutokufanya kazi na sisi ,mko sahihi na sisi pia tuna haki hiyo hiyo kwahiyo na sisi tunachagua kutokufanya kazi na nyie na kuanzia leo video zenu hazitakuwa zinapatikana kwenye mtandao wala channel yetu na pia kuanzia leo tunajivua majukumu yote ya kibiashara na nyie… mmefanya maamuzi na sisi pia tumechukua hatua hiyo, Simple!” <<< SOUNDCITY.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments