Habari za Mastaa

Baada ya Soundcity kujibu kwa nini hawapigi Video za P Square, Manager wao nae kawaandikia haya…

on

Ni siku ya pili toka mgogoro wa P Square na kituo kikubwa cha burudani nchini Nigeria Soundcity TV uwekwe hadharani…

Stori ilianzia pale ambapo Television ya Soundcity TV waliamua kusitisha kuzipiga nyimbo za P Square January 2015 baada ya kutokea kutokuwa na maelewano kati yao mwisho wa mwaka 2014… kauli ambayo hawakuipenda ni ya kaka na Manager wa kundi la P Square, Jude Okoye kusema kuwa Soundcity TV haijawahi kuwafanyia kitu P Square” wakati Soundcity wanadai wao ndio waliokuwa mstari wa mbele kuwapa support yao kwa kipindi cha miaka 10.

Drama bado zinaendelea kati ya P Square na Soundcity TV... baada ya Soundcity kutoa tamko la kwanini nyimbo za P Square hazipigwi kwenye kituo hicho, kaka na manager wa P Square, Jude Okoye ameonekana kukerwa pia na kile walichokisema Soundcity TV, akaingia kwenye ukurasa wake @Twitter na kuwajibu Soundcity.

jude

Manager wa P Square, Jude Okoye.

>>> “@SOUNDCITYtv nyie mnatengeneza pesa kwa kupiga videos za wasanii kwenye kituo chenu, zinawaingizia mamilioni ya pesa, lakini kwenye hayo mamilioni mnayoingiza wasanii hawapati mgao wao, sisi (wasanii na lebo za muziki) hatulalamiki… na mnasema mnatusaidia, msaada upi mnaotupa? Kazi yangu ni kutengeneza videos kazi yenu @SOUNDCITYtv ni kuzicheza… vituo vingine vyenye sifa nzuri havina tatizo kuwalipa wasanii kwenye events zao… mnaweza mkaendelea kuwaonea wasanii wengine lakini sio P Square…” <<< @Judeengees.

Hizi ni baadhi ya tweets za Jude Okoye nilizofanikiwa kuzinasa kupitia page yake ya Twitter

SOUNDCITY1

SOUNDCITY2

SOUNDCITY3

SOUNDCITY4

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments