Habari za Mastaa

Uhakika wa taarifa za Spack aliyewahi kuwa TipTop.

By

on

spack1Usiku wa January 23 zilianza kusambaa taarifa kuhusu Spack,taarifa hizi hazikuwa taarifa njema maana zilisema Spack kapata ajali na kufariki Dunia,millardayo.com iliamua kumpigia simu za spack lakini kwa bahati mbaya hazikupatikana zote.

Ikumbukwe Spack ni moja kati ya wasanii waliokuwa wakiwakilisha familia ya Tip Top Connection ambayo maskani yake ni pale Manzese,hivyo kwa kutumia kigezo hiki tulimpigia simu Madee pengine anaweza kuwa na taarifa zozote lakini nae alisema ndiyo kwanza anasikia kwetu.

Baada ya saa chache mnamo sa 5 usiku tulifanikiwa kumpata Spack mwenyewe ambaye alithibitsha taarifa za kupata ajali na kusema walikua wawili wakitoka Dar es salaam kuelekea Kampala Uganda kwa ajili ya show iliyokuwa ifanyike January 24 siku ya Ijumaa lakini kwa bahati mbaya walipata ajali Jan 23 saa 7 mchana.

Spack bado amelazwa na anadai sehemu alizoumia ni mapaja yake yote mawili na upande wa mtu aliyekua nae kavunjika mkono,chanzo cha ajali hiyo amesema hadi sasa hajakijua ila anahisi mwendo aliyokua anatembea nao.

Msikilize Spack hapa chini kwa kubonyeza play.

Tupia Comments