Hapo jana Washindi wa Lucky Droo ya kwanza iliyofanyika mubashara kupitia ukurasa wa Instagram @infinixmobiletz ambao ni Judithi, Iddy na Omary walikabidhiwa zawadi zao rasmi.
Mshindi wa TV 65″ Bi Grace alikuwa na haya yakusema baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo,
“Nimefurahi sana kwakweli maana nilipopigiwa simu kuwa nimeshinda nikajua ni matapeli ila nikawasiliana na @Infinixmobiletz kwenye ukurasa wao wa Instagram nikahakikishiwa kuwa ni kweli, Japo kuna namna nilikuwa siamini bado mpaka leo nilipokabidhiwa Friji langu, Nimefurahi sana kwakweli na ni mtumiaji mzuri wa simu zaInfinix na sasa natumia Infinix NOTE 12 VIP ni simu nzuriinadumu na chaji kwa muda mrefu pia inajaa chaji kwa dakika17 tu kufikia asilimia 100%’’.
Wakati wa uchezeshaji wa Droo hiyo Afisa Mahusiano InfinixB wana Eric Mkomoye amewataka Watanzania wote na wateja wa Infinix kufika katika maduka yao ya simu, Promosheni ya PIGA UTOBOE inaendelea kuwepo hadi 4/1/2023 ambapo Droo ya pili ya kuwania TV na Fridge itachezeshwa mubashara kupitia infinixmobiletz .
Washindi wameonesha kufurahia zoezi la ukabidhishwaji wa zawadi na huduma zinazotolewa na kampuni hiyo ya simu.