Baada ya udhamini mnono kwa vilabu vya Ligi Kuu soka Tanzania bara, kampuni ya michezo ya ubashiri ya SportPesa leo August 11 2017 imeingia mkataba wa udhamini na club ya Cape Town City ya Afrika Kusini, mkataba ambao unaelenga kuisaidia kusonga mbele club hiyo.
Cape Town City inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini imefanikiwa kuingia mkataba wa miaka minne na SportPesa ambapo kuanzia msimu wa 2017/2018 itaonekana ikivaa jezi zenye neno na logo ya SportPesa ambao ndio wadhamini wakuu wa club hiyo kwa sasa.
Club ya Cape Town City sio club ya kwanza kufaidika na udhamini mnono wa SportPesa, kuna vilabu vingine ambavyo pia vinadhaminiwa na SportPesa kama Everton, Hull City vya England, Simba, Yanga na Singida United vya Tanzania huku ikiwa imedhamini Ligi Kuu Kenya.
Mkataba wa makubaliano ya udhamini huo umesainiwa leo nchini Afrika Kusini, kama hufahamu club ya Cape Town City inayodhaminiwa na SportPesa ni moja kati ya club zinazofanya vizuri katika Ligi Kuu Afrika Kusini na msimu wa 2016/2017 imemaliza nafasi ya tatu.
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0