Top Stories

Spika afanya mabadiliko kwenye kamati mabadiliko ya wajumbe

on

Spika wa Bunge Job Ndugai amefanya mabadiliko madogo ya Wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge kwa kuzingatia matakwa ya kanuni ambapo Godwin Kunambi amehamishwa kutoka kamati ya Mambo ya nje ulinzi na usalama kwenda Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Humphrey Polepole amehamishwa kutoka Kamati ya Utawala na Serikali za mitaa kwenda Kamati ya Sheria ndogo huku Asia Halamga akiteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya masuala ya UKIMWI.

Dr. Faustine Ndugulile ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya sheria Ndogo na Kamati ya masuala ya UKIMWI huku Dr. Medard Kalemani akiteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya sheria Ndogo.

Mwingine ni Dr. Leonard Chamuriho aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya sheria ndogo huku Agnes Marwa akiteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya masuala ya UKIMWI.

.

UTEUZI ULIOFANYWA NA RAIS SAMIA, AMTEUA SOPHIA MJEMA KUWA MKUU WA MKOA SHINYANGA

Soma na hizi

Tupia Comments