Spika wa bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa wanaotumia nguvu na mamlaka kukamata wananchi pasipokuwa na sababu za msingi jambo ambalo amelitaja kuwa ni ukiukwaji wa taratibu za kisheria.
Dkt. Tulia amekemea hilo kufuatua Hoja ya dharura iliyowasilishwa bungeni na mbunge wa Jimbo la Mlimba,Godwin Kunambi akiomba wabunge wenzake kujadili kamatakamata ya kutumia nguvu na mamlaka inayofanywa na wakuu wa mikoa na wilaya nchini huku akihusisha tukio la watu 16 wakiwemo viongozi wa kata na kijiji kukamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro.
“Tarehe 26-08-2024 mheshimiwa DC (Kilombero) akiwa kwenye ziara yake kata ya mbingu kijiji cha Chiwachiwa akienda kusikiliza mgogoro wa ardhi baina ya msitu wa hifadhi ya TFS na na eananchi wa kijiji cha Chiwachiwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara diwani aliweka hoja ya kutaka ku’verify’ hoja hii ilimpelekea DC kusema anamharibia mkutano na akaagiza kamata weka ndani Diwani,mtendaji wa kata,mtendaji wa kijiji na baadhi ya wananchi 11 mpaka sasa navyozungumza wako ndani” mbunge Kunambi
Kufuatia hoja hiyo Spika wa bunge Dkt. Tulia Ackson amemuomba waziri mkuu kufuatilia sababu zilizopelekea kukamatwa kwa watu hao ili bunge na mbunge ajulishwe sababu za watu kukamatwa .
Kwasababu jambo hili sio jambo jipya kwahiyo siwezi kuita ni jambo la dharura isipokuwa kwa changamoto aliyoiwasilisha mbunge serikali ipo humu ndani na mheshimiwa waziri mkuu upo humu ndani na jambo hili limezungumza kwa kirefu basi huyo DC na Mkuu wa mkoa hebu tufahamu changamoto iko wapi ili sheria itekelezwe kwa namna bunge linavyotaka kwasababu bunge limetoa nafasi kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya hivyo pale ambapo wanaona huyu mtu anayeagizwa akamatwe anahatarisha usalama wa watu walioko pale au yeye mwenyewe usalama wake unahatarishwa”