Top Stories

Spika wa Bunge aamuru Wabunge kuvaa barako Marekani

on

Leo July 30, 2020 Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi ameamuru kuwa wabunge na wafanyakzi wote wa chombo hicho watapaswa kuvaa barakoa katika kipindi chote cha janga la virusi vya corona.

Akizungumza bungeni jana, Pelosi amesema anatumai wabunge na wafanyakazi wote wanaheshimu sharti hilo kama ishara ya kulinda afya na usalama wa kila mmoja ndani ya majengo ya Bunge.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya mbunge wa chama cha Republican Louie Gohmert aliyepinga vikali uvaaji barakoa kutangaza kuwa ameambukizwa virusi vya corona jana Jumatano.

Kulingana na Pelosi, chini ya kanuni hiyo mpya wabunge wataruhusiwa tu kuondoa barakoa wakati wa kuhutubia au kutoa michango mbele ya Bunge.

Via DW Swahili

MAGUFULI AWAACHA HOI VIONGOZI MSIBANI WAKIWA NA MAJONZI KUHUSU ATAKAPOZIKWA MWINYI

Soma na hizi

Tupia Comments