Spika wa Bunge Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (African Geopolitical Group of IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameongoza kikao cha Maspika, Wakuu wa Misafara na Wakuu wa taasisi mbalimbali za Afrika ili kupokea maoni kuhusu kuboresha ushiriki wa Mabunge ya Afrika katika shughuli na mikutano ya IPU.
Kikao hicho kimefanyika leo Machi 9, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Exhibition World Bahrain Nchini Bahrain kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).