Michezo

Sporting Lisbon wampa heshima Ronaldo

on

Club ya Sporting Lisbon ya Ureno ambayo ndio club iliyomtoa staa wa Juventus Cristiano Ronaldo enzi za utoto, leo imetangaza kumpa heshima ya kipekee.

Sporting Lisbon imeripotiwa kuwa kwa heshima ya mchezaji huyo sasa wanabadili jina la Academy yao na kuwa “Academia Cristiano Ronaldo” kutokana na heshima ya Ronaldo.

Ronaldo alijiunga na Sporting Lisbon ya kwao Ureno akiwa na umri wa miaka 12, mwaka 1997-2002 na alipokuwa na umri wa miaka 17 ndio akapandishwa timu ya wakubwa hadi 2003 kisha kujiunga na Man United.

Soma na hizi

Tupia Comments