Ad
Ad

Michezo

Headlines 5 za stori kubwa za michezo Uingereza December 10 2015, huyu ndio kocha aliyefutwa kazi ..

on

Imekuwa ni kawaida kwa siku hizi kukuta habari mpya kila siku zikiingia katika headlines, iwe siasa, uchumi au michezo, December 10 nimekukusanyia Top 5 ya stori kubwa za michezo zilizoingia katika headlines, yaani ndio zinatajwa kuandikwa sana December 10, huu ni mkusanyiko wa stori 5 za soka zilizoingia katika headlines December 10.

5-  David Ospina anataka kuondoka Arsenal

David-Ospina2

David Ospina

Hii ni moja kati ya stori zilizoandikwa December 10 kuhusu golikipa wa Arsenal David Ospina kuwa yupo katika mazungumzo na klabu ya Besiktas  ya Uturuki ili ahame Arsenal, golikipa huyo wa Colombia ambaye anaonekana kukosa nafasi katika kikosi cha Arsenal kutokana na uwepo wa Peter Cech huenda akahamia Besiktas .

4- Klabu ya PSG imeingia katika mbio za Chelsea za kuwania saini ya Aubameyang

Pierre-Emerick-Aubameyang

Pierre-Emerick Aubameyang

 Klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa imeingia katika mbio za vilabu vya Chelsea, Liverpool na Manchester United ya kutaka saini ya  mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. Jose Mourinho na Jurgen Klopp ndio kwa kiasi kikubwa wanataka kumsajili staa huyo wa Gabon aliyecheza jumla ya mechi 22 za mashindano yote msimu huu akiwa Borussia Dortmund na kufunga magoli 25.

3- Van Gaal anaweza kufukuzwa kama?

Louis-van-Gaal-anxiety

Louis van Gaal

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal anatajwa kupewa onyo na uongozi wa Man United kama hatomaliza T0p 3 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza basi atafutwa kazi, licha ya kuwa taarifa hizo hazijawekwa hadharani ila kutolewa kwa Man United katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya katika hatua ya Makundi kumechangia hilo.

2- Kocha wa Swansea City Garry Monk amefutwa kazi

Monk-sacked

Garry Monk

Uongozi wa klabu ya Swansea City umetangaza kumfuta kazi Garry Monk, uamuzi huo umekuja baada ya Monk kuifundisha Swansea kwa miezi 22. Monk mwenye umri wa miaka 36 alifanya vizuri msimu uliyopita kwa kuiongoza Swansea kuifunga Man United nyumbani na ugenini pamoja na kuifunga Arsenal.

1- Moura anataka kuhamia Arsenal

Lucas-Moura1

Lucas Moura

Winga wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Lucas Moura anatajwa kuthibitisha kuwa anapenda kucheza Ligi Kuu Uingereza hususani katika klabu ya Arsenal kuliko klabu ya Liverpool ambazo zote amekuwa akihusishwa nazo. Moura anaripotiwa kumpenda kocha wa Arsenal Arsene Wenger na angependa kufanya kazi chini ya kocha huyo.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments