Michezo

Kauli za wasemaji wa Simba na Yanga kuhusu mechi za Ligi Kuu kuchezwa saa 9 alasiri (+Audio)

on

September 18 ni siku ambayo headlines za Bodi ya Ligi kutaka kubadilisha muda wa kuanza kwa mechi za Ligi Kuu soka Tanzania bara zilizidi kuchukua nafasi kwa kila mdau au mshabiki wa soka kuzungumza maoni yake juu ya uamuzi huo unaotarajiwa kufanywa muda wowote kutokea hivi sasa.

millardayo.com ilipata nafasi ya kufanya exclusive interview na wakuu wa idara za habari za klabu za Simba na Yanga, Haji Manara wa Simba na Jerry Muro wa Yanga, kubwa tulitaka kufahamu  uamuzi na mtazamo wao juu ya mabadiliko hayo ya muda wa kuanza mechi za Ligi Kuu kuwa ziwezinachezwa saa 9 badala ya saa 10 au saa 10 na nusu.

DSC_0161

Haji Manara afisa habari wa Simba.

“Msimamo wa Simba katika hili hatukubaliani nalo kwani mechi kuchezwa saa 9 maana yake nini? maana yake kwamba utapunguza kwa kiasi kikubwa mapato ya klabu, klabu zetu hizi kwa kiwango kikubwa zinategemea mapato ya mlangoni ili ziweze kujiendesha, bado hatujaweza kuwa na vyanzo vingi vya mapato”>>> Haji Manara

“Vitu kama hivi vinachanganya kwanza kuleta jambo wakati Ligi tayari imeshaanza, nafikiri sio jambo la msingi katika maendeleo ya mpira wetu lakini lingine nikilitazama kwa makini zaidi haingii akilini kupeleka wachezaji uwanjani saa 7, saa 8 tuanze warm up na saa tisa mechi ianze, ukiangalia muda huo ni jua kali sana”>>> Jerry Muro

DSC_0155

Jerry Muro afisa habari wa Yanga

Hii ni sauti ya Haji Manara na Jerry Muro

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments