Michezo

Sentensi mbili alizosema Jonas Mkude baada ya kusaini upya Simba

on

Screen Shot 2014-11-13 at 10.41.57 AMBaada ya kizungumkuti cha takribani miezi mitatu juu ya mkataba mpya na klabu yake ya Simba, hatimaye kiungo Jonas Mkude amefanya kitendo ambacho kitawafurahisha mashabiki wengi wa Simba.

Kiungo huyo ambaye alikuwa anatajwa kuwa kwenye listi ya wachezaji ambao wangesajiliwa na Yanga mwezi January, November 12 2014 amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea simba na kusema: “Bado nipo sana Msimbazi”

Amesaini mkataba huo Jana mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva na viongozi wengine wa Simba akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya ssajili ya Simba, Zacharia Hans Pope.

IMG_8754.JPGBaada ya kusaini mkataba huo Mkude alisema “Nafurahi kusaini Simba SC, klabu ambayo imenikuza kisoka tangu timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 hadi leo, nawaahidi wana Simba SC kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuiletea mafanikio klabu yangu”

Tupia Comments