Kulipiza kisasi itakuwa mada kuu katika msimu wa pili unaotarajiwa sana wa ” Squid Game,” kulingana na mtayarishaji Hwang Dong-hyuk ikipambwa na waigizaji wakubwa na changamoto za kusisimua zaidi kuliko msimu wa kwanza.
Akizungumza katika hafla ya fupi huko Lucca, Italia, Hwang alisema kwamba msimu wa tatu tayari uko katika utayarishaji na akadokeza kuwa toleo la lugha ya Kiingereza linaweza pia kutengenezwa.
Msimu wa kwanza, uliotolewa mnamo 2021, ukawa mfululizo uliotazamwa zaidi wa Netflix.
Muendelezo wa Squid Game 2 unatazamiwa kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Desemba 26, huku msimu wa tatu ukitarajiwa 2025.
Hwang alieleza, “Katika Msimu wa 2, Gi-hun, ambaye alinusurika Msimu wa 1, atarejea kwenye michezo, si kushinda wakati huu, lakini kukomesha michezo hii.” Aliongeza, “Kutakuwa na idadi kubwa ya wahusika wakati huu na michezo ya kufurahisha zaidi.”
Hivi majuzi, Netflix ilidondosha TRAILER rasmi ya Squid Game: Msimu wa 2 kwenye YouTube, lakini muhimu tarajia kuona mengi kwenye Season 2 ya SQUID GAME