Mix

Maneno ya aliyetobolewa macho na Scorpion baada ya kudaiwa kutelekeza mke

on

Saidi Mrisho ambaye ali-make headline siku za nyuma baada ya kutobolewa macho na mtu anayefahamika kwa jina la Salum Njwete maarufu kama ‘Scorpion’ amerudi tena kwenye headlines mara hii ikiwa ni issue nyingine akidaiwa kuitelekeza familia.

Kupitia Leo Tena ya Clouds FM leo July 13, 2017 Said anadaiwa kumtelekeza mkewe ambaye amejifungua watoto mapacha hivi karibuni huku akikiri kuachana na mke wake huyo kutokana na tofauti zilizotokea kati yao na kusisitiza kuwa hajatelekeza familia yake.

>>>”Ni kweli nimeachana na mke wangu ambaye nimefunga naye ndoa hivi karibuni baada ya kupata matatizo ila sijatelekeza familia. Hii ndoa nimefunga kutokana na shinikizo kutoka kwa wazazi wa mke wangu ili tukiachana tuweze kugawana vifaa vilivyokuja. Japokuwa tumeachana lakini nimempangia nyumba na namsaidia kwa sababu nina familia naye. Kwa sasa nimeoa mke mwingine.

“Mke wangu nimemuacha sababu ya tabia zake. Mwanzoni nikiwa naona alikuwa akinisaliti lakini hata sasa anaendelea kunisaliti. Siku moja aliniomba simu akaniambia ampigie mtu aliyemkopesha pesa Hospitali.

“Nilimpatia simu mama akatoka lakini alichelewa kurudi nikamuuliza vipi akasema alikuwa hapatikani lakini baadaye nikabonyeza button ya kupiga. Nilipopiga simu akapokea mwanaume mwingine nikamuuliza vipi akaniambia huyu ni mke wake kivipi wakati ni mke wangu mimi. 

“Mke wangu amenifanyia vitu vingi vya ajabu anapigiwa simu na wanaume na hao wanaume wananitukana. Nilimueleza baba yake akaniambia nimpe talaka au nimuoe mwanamke mwingine. Amekuwa mlevi. Anaweza hata kumuingiza mwanaume mwingine chumbani kwangu kwa sababu sioni. Kwa kweli nilishindwa kuvumilia hasa kutokana na hali yangu.” Said.

Hata hivyo. naye mke wa Said maarufu kama Mama Dee amesema yote yaliyosemwa na Said siyo kweli kwani alimpangia nyumba sehemu nyingine na kumdanganya kisha akaenda kuoa mwanamke mwingine wakati wa Ramadhan.

>>>“Sababu anazozitoa Baba Dee ni uongo hakuna jambo lenye ukweli hata kidogo. Kinachoshangaza Saidi alitafuta nyumba nyingine tena akahamisha vitu kule kwenye nyumba ya Tabata lakini mimi alinidanganya. Nilipomuuliza Makabati yako wapi akasema yapo kwa Fundi nimeyapeleka kupakwa rangi kumbe muongo kampangisha mwanamke ambaye amemuoa mwezi wa Ramadhan.” – Mama Dee.

VIDEO: Aliyetobolewa macho alivyofika mahakamani kutoa ushahidi kesi ya Scorpion

Soma na hizi

Tupia Comments