Michezo

Staa wa Man United kwenye headlines na mpenzi wa zamani wa Chris Brown (+Pichaz)

on

Winga wa kimataifa wa Uholanzi anayekipiga katika klabu ya Manchester United Memphis Depay, ameingia kwenye headlines na mpenzi wa zamani wa staa wa muziki wa Marekani. Memphis Depay ambaye amejiunga na klabu ya Manchester United katika majira ya usajili yaliyofungwa mwezi August mwaka huu akitokea klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi,  Depay ameonekana akiwa pamoja na mpenzi wa zamani wa Chris Brown.

2CDED5CD00000578-0-image-a-54_1443468846612

Depay ameonekana akikatiza sehemu kadhaa akiwa pamoja na mwanamitindo Karrueche Tran ambaye aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na staa wa muziki wa Marekani Chris BrownKarrueche Tran amewahi kuingia katika headlines mara kadhaa na Chris Brown baada ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi ya kuachana na kurudiana.

2CDECF7100000578-0-image-a-55_1443469034106

Kwa sasa Karrueche Tran yupo karibu sana na staa wa klabu ya Manchester United Memphis Depay kitu ambacho kinafanya wengi wajiulize maswali kuhusiana na ukaribu huo. Depay na Karrueche Tran wameonekana pamoja wakiwa sehemu kadhaa ikiwemo Club LIV. Hii sio mara ya kwanza kwa Depay kuonekana akiwa pamoja na Karrueche Tran kwani waliwahi kuonekana katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa msimu huu.

2CDED0F800000578-3252567-image-a-5_1443471119549

2CDF3DD400000578-3252567-image-a-71_1443469920752

Hii ndio picha ya kwanza ambayo walionekana pamoja kati kati ya mwaka huu Depay na Karrueche Tran

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Tupia Comments