Michezo

Full Time ya Taifa Stars Vs Algeria November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam (+Pichaz)

on

Hatimaye mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika Urusi kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Algeria Mbweha wa Jangwani ndio umechezwa leo November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, mchezo wa marudiano utachezwa November 17 Algiers.

DSC_0111

Mbwana Samatta akijaribu kumtoka Mandi Issa wa Algeria

Takwimu za mchezo huo zilikuwa rafiki kwa upande wa timu zote mbili kwani kabla ya kupigwa mchezo huo, kwa takwimu za hivi karibuni Taifa Stars iliwahi kucheza na Algeria September 3 2010 Algiers na kutoka 0-0 katika mchezo wa AFCON, lakini September 3 2011 Dar Es Salaam Stars ilitoka sare ya goli 1-1 kitu ambacho kilifanya timu zote kuwa na rekodi ambazo haziwezi kumtisha mwenzake.

DSC_0120

Farid Mussa akipiga mpira ambao ulizuiliwa kwa mkono na Mandi Issa ila haikuwa penati

Licha ya kuwa Taifa Satrs ilikuwa katika nafasi za chini katika viwango vya FIFA ukilinganisha na Algeria, hiyo haikuifanya Taifa Stars ishindwe kucheza soka safi, kipindi cha kwanza Stars ilianza kwa kukosa magoli kabla ya dakika 43 Elias Maguli kupachika goli la kwanza ambalo lilidumu kwa dakika zote 45.

DSC_0083

Mashabiki hawakuacha kuwapongeza wachezaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kipindi cha pili Taifa Stars walirudi kwa kasi na Mbwana Samatta akadhihirisha ubora wake wa kupachika magoli baada ya dakika 54 kupachika goli la pili kwa Stars, furaha ya watanzania ilianza kupotea dakika ya 71, baada ya Sliman Islam kupachika goli la kwanza kwa Algeria na dakika mbili mbele akapachika goli la pili, hadi dakika 90 zinamalizika Taifa Stars 2-2 Algeria.

DSC_0106

Wachezaji wa Taifa Stars wakifurahia goli la Mbwana Samatta

DSC_0064

Thomas Ulimwengu katika harakati za kumpita Ghoulam Faouzi wa Algeria

DSC_0075

Elias Maguli na Nadir Haroub wakifurahia goli la kwanza la Taifa Stars

DSC_0085

Mashabiki wa Tanzania wakati wa mapumziko walivyokuwa wanafurahia goli la Maguli

DSC_0058

Thomas Ulimwengu akijaribu kumtoka Mandi Issa wa Algeria

DSC_0052

Kocha wa makipa Peter Manyika Senior akisali na golikipa wa Taifa Stars Ally Mustapha kabla ya mchezo kuanza

DSC_0097

Mbwana Samatta akishangilia goli baada ya kufunga

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.

Tupia Comments