Michezo

Duu!!! Kama Taifa Stars wakiifunga Algeria, wachezaji watavuta mkwanja mrefu, hili ndio dau watakalopewa …

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars bado haina hali nzuri sana ya kujihakikishia inashinda mchezo wake wa marudiano dhidi ya Algeria, baada ya mchezo wa kwanza uliyochezwa November 14 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kumalizika kwa sare ya goli 2-2, matokeo hayo hayatajwi kuwa mazuri sana kwa Taifa Stars ukilinganisha wanaenda kucheza ugenini.

Taifa Stars ambayo imesafiri leo November 15 kuelekea Algeria tayari imewasili salama lakini imeahidiwa milioni 500 na kamati ya ushindi ya Taifa Stars, kamati hiyo imetangaza dau hilo kama motisha kwa wachezaji ili waweze kucheza na kupata matokeo mazuri, mchezo wa kwanza Taifa Stars waliahidiwa milioni 50 kama wangeshinda ila wamepewa milioni 25 baada ya kutoa sare.

DSC_8434

Kiwango kilichotangazwa na kamati ya ushindi ya Taifa Stars ni mara kumi ya dau walilokuwa wameahidiwa awali, hivyo hii ni jinsi ambavyo kamati ya ushindi imeipa uzito mechi hiyo, majirani wa Tanzania timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kuwa timu ya kwanza ya Afrika Mashariki kufuzu hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi. Taifa Stars itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya Algeria Jumanne ya November 17 Algeria.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.

Tupia Comments