Michezo

Hawa ndio wachezaji 22 wa Taifa Stars watakaokwenda kuweka kambi Uturuki…

on

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars  Charles Boniface Mkwasa August 21 ametangaza kikosi cha wachezaji 22 watakaosafiri kwenda kuweka kambi ya siku 8 Istanbul Uturuki. Mkwasa ametangaza kikosi hicho ambacho kila mchezaji aliyeitwa anatakiwa kuripoti saa 5 asubuhi siku ya Jumapaili August 23 tayari kwa safari usiku wake.

IMG_201506175_012610

Taifa Stars inakwenda kuweka kambi Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kuwania kucheza AFCON 2017, mechi ambayo itachezwa Septemba 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, orodha hiyo ya wachezaji 22 imetangazwa kutoka katika kikosi cha awali kilichotangazwa wiki mbili mbili nyuma.

DSC_0022

Wachezaji waliochaguliwa ni

All Mustafa (Yanga SC)

Aishi Manula (Azam FC)

Said Mohamed (Mtibwa Sugar)

Shomari Kapombe (Azam FC)

Abdi Banda (Simba SC)

Mohamed Hussein (Simba SC)

Hassan Isihaka (Simba SC)

Juma Abdul (Yanga SC).

Haji Mngwali (Yanga SC).

Kelvin Yondani (Yanga SC).

Nadir Haroub (Yanga SC).

DSC_0021

Mudathir Yahya (Azam FC)

Himid Mao (Azam FC)

Frank Domayo (Azam FC)

Salum Telela (Yanga SC)

Deus Kaseke (Yanga SC)

Said Ndemla (Simba SC)

John Bocco (Azam FC)

Farid Musa (Azam FC)

Rashid Mandawa (Mwadui FC)

Simon Msuva (Yanga SC)

Ibrahim Ajib (Simba SC)

Taifa Stars inatarajiwa kuondoka jumapili usiku kwa usafiri wa shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines), na kufika Jumatatu asubuhi jijini Istanbul, ambapo timu itaelekea katika mji wa Kocael ambapo itaweka kambi ya wiki moja katika hoteli ya Green Park Kartepe.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments