Michezo

Picha: Beki wa klabu ya Inter Milan atua Tanzania, afika Serengeti kushuhudia vivutio

on

Beki wa Inter Milan ya Italia na nahodha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Uholanzi Stefan de Vrij amewasili Tanzania kwa ajili ya mapumziko na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii.

Stefan de Vrij anaingia kwenye orodhaa ya wachezaji wa soka waliofika kuitembelea Tanzania  2022 hususani kwenye upande wa vivutio akiwemo, mchezaji wa klabu ya PSG Ander Herrera na wa Liverpool Ibrahima Konate.

Kwa mujibu wa Waongoza Watalii kutoka Ebony Tours Safaris alisema..’Hii ni kubwa sana kwa nchi yetu kwani na wapo wachezaji wengi waliowahi kufika nchini sema wengine hawapendi kuwa kwenye mitandao kwani wanakuwa na mambo yao binafsi ila kwa Stefan De Vriji alivutiwa na vivutio vyetu vya Tanzania’- Aboud

‘Kwasasa yupo Serengeti pia aliomba apelekwe Zanzibar kujionea vivutio mbalimbali hii inatupa majibu tosha kwamba Filamu ya Royal Tour ya Rais Samia imesaidia kuujulisha ulimwengu wote Duniani na hatimae Tanzania inaenda kuweka rekodi tofauti katika masuala ya Utalii’- Aboud

Tupia Comments