Habari za Mastaa

Wasanii walivyojipanga kutekeleza agizo la Rais MAGUFULI Dec 9…..

on

Ikiwa ni siku kadhaa tangu Rais wa awamo ya tano Dk.John Magufuli kutoa tamko la hakutakua na sherehe za kitaifa December 9 na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao.

Sasa time hii headlines za usafi zimewagusa wasanii na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda ambapo tarehe 9 December wataungana kuhakikisha wilaya ya Kinondoni usafi unafanyika kwenye maeneo mbalimbali.

Akiongea na ripota wa millardayo Steve Nyerere alisema..’Kutakuwa na wasanii mbalimbali ambao tutaungana siku ya usafi katika wilaya ya Kinondoni pamoja na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, watu wengi wanaamini usafi ni lazima ma hospitali lakini usafi unaanzia nyumbani kwako, masoko na sehemu mbalimbali zinazomzunguka mwanadamu’ – Steve Nyerere

‘Napenda kusema kwamba siku hiyo wasanii pamoja na wananchi tujitokeze kutekeleza kile kilichosemwa na Mh Rais wa awamo ya tano Dk.John Pombe Magufuli tujitokeze kwa wingi  kufanya usafi huu ni mfano wa kuigwa kwenye mataifa haya ya Afrika’>> Steve Nyerere

Wapo wasanii kama 180  mimi nikiwa kama kiongozi wao na Mh DC Paul Makonda  tumechagua wasanii mbalimbali wakiwemo wasanii wa Bongo Movie, Bongo Fleva, wanenguaji kwa hiyo tumechagua vitengo vyote vya sanaa kuhakikisha usafi unafanyika katika wilaya ya Kinondoni’>> Steve Nyerere

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana naMillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments