Habari za Mastaa

Na Steve Nyerere ametangaza rasmi anautaka Ubunge 2015, maneno yake ninayo hapa

on

.

.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Nyerere ameingia kwenye list ya wagombea ubunge mwaka 2015

Kwenye interview na millardayo.com Steve amesema Kwanza ninataka kuwahakikishia watanzania sijakurupuka, nimekuwa  mwanachama wa chama cha Mapinduzi  umoja wa vijana almost miaka 25 na sasa hivi nina miaka 29 naelekea 30 lakini vilevile nimekuwa kamanda wa vijana miaka 10 tawi la bwani kinondoni, nimekuwa muhamasishaji  wa chama cha mapinduzi kitaifa kwa muda wa miaka 10′

‘Sijakurupuka na wala sijatamkia sifa kwasababu labda nimeona mtu fulani amegombea, kinondoni kuna matatizo kadhaa  nani anaweza kuyatetea hayo matatizo? nitakuwa mtetezi pamoja na matatizo ya wasanii wetu, kuhusu kazi zangu za filamu nitakuwa nafanya kama kawaida huku nikiwa natumikia kazi za Bungeni’

ATAACHA KUIGIZA?!

Amejibu >>> ‘Kazi yangu ya sanaa sitoweza kuiacha nadhani naweza kuwa ndio Mbunge wa kwanza yuko ndani ya Bunge na bado yuko kwenye sanaa anacheza filamu’

Unaweza ukasikiliza alichokizungumza Steve Nyerere kwa kubonyeza play hapa chini

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments