Madaktari watano kutoka Tanzania wamejitolea kwenda nchini Sierra Leone na Liberia kutoa huduma kwa wagonjwa wa ebola.
Madaktari hao ambao ni wataalam wa magonjwa ya milipuko waliondoka nchini jana na Shirika la ndege la Ethiopia na wanatarajia kuwepo katika nchi hizo kwa miezi mitatu mfululizo,
Mganga mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya Dolnald Mmbando aliwataja madaktari hao kuwa wanatoka katika hospitali za Morogoro,Lindi,Mbeya na wengine kutoka ndani ya Wizara hiyo.
NIPASHE
Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee aliachiwa huru jana na wenzake baada ya kulala Segerea siku moja na kusema aliishi vizuri na kula ‘bata’ ambalo hajawahi kula maishani mwake akiwa gerezani humo.
Mdee na wenzake wanane waliachiwa huru na mahakama ya Kisutu baada ya kutimiza masharti ya dhamana katika kesi ya kupinga amri halali ya Jeshi la Polisi na kukusanyika isivyo halali kwa lengo la kwenda Ikulu.
Baada ya kuachiwa Mdee alisikika akisema kama Serikali ilidhani imemkomoa kwa kumlaza Segerea ni sawa na bure kwa sababu amekula bata ambao hajawahi kula na kama alikua anachechemea sasa anakimbia kutokana na kujiamini zaidi.
Katika viunga vya mahakama hiyo wafuasi mbalimbali wa Chadema walionekana kufurika kwa wingi huku ulinzi mkali wa polisi pamoja na mbwa ukiimarishwa katika eneo hilo.
MWANANCHI
Shule ya Sekondari ya wavulana Njombe imefungwa kwa muda wa mezi mmoja kuanzia jana baada ya wanafunzi kuchoma moto bweni,karakana na kuharibu mali mbalimbali za shule na za walimu.
Uamuzi wa kuifunga shule ulitolewa jana na Ofisa elimu wa Mkoa wa Njombe Said Nyasiro baada ya kufika katika eneo la tukio na kujionea madhara yaliyotokea huku akiagiza wanafunzi hao kurejea shuleni hapo na wazazi wao pamoja na kiasi cha shilingi 150,000 kila mmoja.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kwa zaidi ya saa mbili ili kuwatuliza huku wakazi wanaoishi jirani na shule hiyo wakiwa wamejawa hofu kutokana na vurugu hizo.
Chanzo cha wanafunzi kuchoma bweni inasadikiwa ni baada ya wenzao 30 kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu ikiwamo kutoroka na kwenda disko usiku.
MWANANCHI
Moja ya mambo ya kushangaza katika jiji la Mbeya ni matukio ya kufunga ndoa kwa siku zote saba za wiki bila kujali siku za kazi ama za ibada.
Watu wamezoea kuona harusi zikianza kufungwa kuanzia ijumaa mpaka jumapili katika Mikoa mbalimbali lakini kwa Mbeya imekua tofauti na harusi hufungwa kuanzia jumatatu mpaka jumapili kutokana na uhaba wa kumbi za kufanyia sherehe.
Katika Mitaa mbalimbali ya Mbeya ni kawaida kwa siku za jumatatu hadi jumapili mambo ya arusi kuanza saa5.00 asubuhi hadi saa12.00 jioni jambo ambalo ni la kawaida.
Baadhi ya wamiliki wa kumbi za harusi wamekiri kupokea oda za arusi mara nne hadi tano kwa wiki na kwa miezi hii nafasi zimejaa sehemu mbalimbali mpaka mwakani.
HABARILEO
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Willium Lukuvi amemtaka Katibu mkuu wa CCM Abdulrhman Kinana kuhoji utendeji kazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.
Ombi la Lukuvi kwa Kinana linatokana na kile kinachosemekena ni kitendo cha Nyalandu kutojibu barua mbili alizoandikiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Christine Ishengoma kuhusu malalamiko ya wananchi wake dhidi ya mwekezaji wa kampuni ya utalii wa uwindaji ya Kilombero North Safaris.
Lukuvi alisema wananchi hao walimlalamikia na kumtaka kumfikishia ujumbe Waziri huyo ili aweze kuwatatulia kero hiyo lakini pamoja na kumwandia barua hajajibu lolote mpaka sasa.
“Ni vyema ukatuita wote ili tujue tatizo liko wapi nadhani wewe Kinana ukimwita utamfundisha kuwa viongozi wenzake wakimwandikia barua anapaswa kuwajibu na kuwasaidia wananchi malalamiko yao”alisema Lukuvi.
HABARILEO
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imeruhusu mashindano ya Miss Tanzania kufanyika jumamosi kama ilivyopangwa awali na uongozi wa shindano hilo.
Hakimu Frank Mosha alitoa agizo hilo baada ya kusikiliza ombi lililowakilishwa na mwanzilishi wa mashindano hayo Prashant Patel dhidi ya mshirika wake Hashimu Lundenga.
Akitoa uamuzi huo Mosha alisema hakuna sababu ya kuzuia mashindano hayo kufanyika kwa kuwa akitoa amri hiyo itaathiri watendaji pamoja na watu wengine ikiwemo wadhamini.
UHURU
Watanzania zaidi ya 400,000 wamebainika kuwa na magonjwa ya akili huku jiji la Dar es salaam likiwa kinara kwa kuwa na watu wengi zaidi.
Pamoja na idadi hiyo kubwa bado wagonjwa wamekua hawajitambui na hata wale wanaojitambua hawafiki kwenye vituo vya afya kupata huduma.
Waziri wa Afya Dk Seif Rashid alisema kwa kujibu wa takwimu za taarifa za afya ya akili mwaka jana na mwaka huu jiji la Dar ndio kinara wa kuw ana silimia mbili ya wagonjwa wote nchini.
Alisema zipo sababu mbalimbali zinazosababisha watu wenye uchizi kupoteza uwezo wao wa kujitegemea kama kupoteza uwezo wa kufikiri na kutopata usingizi.
Alisema miongoni mwa dalili za uchizi ni mtu kuwa na tabia za ajabu,kusikia sauti na kuona vitu ambavyo havipo,kujiona maarufu na kujiona wao ndio manabii wa kweli.
TABIBU
Ugonjwa hatari wa Marburg ni homa hatari inayoendana na ugonjwa wa ebola kwani virusi vya magonjwa hayo ni ya jamiii moja ijulikanayo kama Filoviridae.
Ugonjwa huo umeonekena kuanza kuzitisha nchi za Afrika Mashariki na kati na kuenezwa na mnyama aina ya popo ambao ndio husambaza virusi vyake na maambukizi baina ya binadamu hutokana na kugusana.
Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na mtu kuwa na homa ya gafla ya kiwango cha juu cha joto,maumivu ya kichwa,maumivu ya viungo na misuli pamoja na kutapika damu.
UHURU
Madaktari waliokua wakimtibu mwanamke mmoja nchini Colombia aliyekua akilalamika kuumwa tumbo wamebaini alikua ameweka kiazi ndani ya uke wake akiogopa kubeba mimba.
Mwanamke huyo miaka22 alidai kushauriwa na mama yake kutumia njia hiyo ili asipate mimba lakini wakati madaktari wakigundua kiazi hicho kilishaanza kuchipua na kuota mizizi ndani ya mwili wake.
Hata hivyo baada ya madaktari kukiondoa kiazi walithibitisha hapakua na madhara makubwa kwa afya ya mwanamke huyo huku wakitoa lawama kwa mama mzazi wa binti huyo kwa kumpotosha mwanaye
MWANANCHI
Mahakama kuu Kenya imeliamuru Baraza kuu la Mitihani nchini humo libadilishe jina na jinsia kwenye cheti cha mlalamikaji mwanaume ambae amekua akipigania atambuliwe kama mwanamke.
Jaji Weldon Korir juzi aliagiza Baraza hilo limpe cheti kipya Andrew Mbugua alilibadilisha jina lake na kuwa Audrey Mbugua baada ya kubadilisha jinsia na kuwa mwanamke katikati ya mwaka jana.
Mbugua alilishtaki baraza la Mitihani kwa kukataa kubadilisha jina lake kwa kuondoa neno mwanaume na kuandika mwanamke hata baada ya kuonyesha gazeti la Serikali likiwa limebadilisha jina lake.
Hata hivyo jaji wa mahakama hiyo ameangalia kesi nyingine za aina hiyo na kufikia maamuzi kwamba zote zinaegemea haki na heshima kwa binadamu.
Unataka stori kama hizi zisikupite? unataka kuwa kupata kila kinachonifikia? karibu ujiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram Facebook