Magazeti

Stori 7 hot kutoka kwenye magazeti ya leo October 10 2014

on

hotnews 1HABARILEO

Watu saba wameuawa na nyumba zaidi ya 20 kuteketezwa kwa moto katika vurugu zinazodaiwa kuanzishwa na wanakijiji Wilaya ya Kasulu chanzo kikiwa imani za kishirikina ambapo habari zilizothibitishwa na Polisi zinasema vurugu hizo zilitokea juzi usiku na watu waliouawa walikua wakituhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo.

Kufuatia hali hiyo watu 18 akiwemo Mwenyekiti wa kijiji aliyeongoza mauaji hayo wanashikiliwa na polisi.

HABARILEO

Sekretarieti ya viongozi wa umma imeamuru Polisi kumkamata mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo na kumfikisha mbele ya baraza la maadili ambapo balozi Jaji mstaafu Hamis Msumi alisema wanao uhakika kiongozi huyo alipokea hati ya kuitwa  katika baraza hilo na alitakiwa kufika jana lakini hakutokea.

Alisema atakapofikishwa mbele ya mahakama ataelezwa ni kwa jinsi gani anatuhumiwa na baraza kutumia madaraka aliyonayo vibaya.

MWANANCHI

Wazazi wa mtoto Mazoea mkazi wa Rufiji wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumtupa mtoto huyo kwenye jiko lenye moto wakimtuhumu kuiba shilingi 6000 za jirani yao, Kamanda wa Polisi alisema wazazi hao wanashikiliwa kwa kosa hilo na watapandishwa kizimbani  leo kujibu tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa ofisa Mtendaji wa kijiji cha Kilimani alisema watuhumiwa hao walifanya kosa hilo baada ya mmoja wa majirani zao kudai ameibiwa kiasi hicho cha fedha ambapo baba yake alimshika miguu na mama yake mikono kisha wakamtupa ndani ya jiko na kuungua vibaya mkono wa kulia wakidai wanamwadhibu kutokana na tabia yake mbaya.

MWANANCHI

Mkazi wa kijiji cha Buriba kata ya Sirari Tarime Buninge Chacha amenusurika kufa baada ya kupigwa mshale kwenye makalio na kuvuja damu nyingi na mtu anayedaiwa kuwa ni mume wake.

Inadaiwa mke wake huyo alikua akipinga binti yao kuozeshwa hali iliyopingwa na mumewe ambae alikasirika na kuamua kumchoma kwa mshale wakati akikimbia kujiokoa, Mwanamke anasema kitendo cha mumewe kumchoma mshale wakati akitetea haki ya mtoto wao kimemfanya aogope kurudi nyumbani kwa madai mumewe anaweza kumuua hivyo ameamua kuishi kwa dada yake.

MTANZANIA

Mahabusu aitwae Andaluswe Mwakapila mkazi wa Olongo Mbeya amejinyonga na kufariki dunia akiwa ndani ya mahabusu katika kituo kidogo cha Polisi Inyala ambapo Kamanda wa Polisi  Mbeya Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema mwili wa marehemu ulikutwa unaning’inia katika dirisha la chumba cha mahabusu.

Alijinyonga kwa kutumia shati lake ambapo chanzo cha kujiua inasemekana kabla ya kufikishwa mahabusu  alikua na ugomvi na mkewe ambapo alimpiga kwa kutumia shoka na jembe na kumsababishia majeraha mengi.

MTANZANIA

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe linawashikilia wanafunzi 15 wa shule ya Sekondari Njombe kwa tuhuma za kuchoma samani za shule na kufanya vurugu kubwa ambapo Kamanda wa Polisi Njombe Flugence Ngonyani alisema Wanafunzi hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Alisema wanafunzi hao wanatuhiumiwa kuchoma mali za shule, vifaa mbalimbali vya wanafunzi, kuvunja duka la shule na kuvunja vioo vya nyumba ya mwalimu huku thamani ya mali zote ikitajwa kuwa milioni 113.

UHURU

Serikali inaangalia uwezekano wa kuongeza mbele umri wa kustaafu kwa wenye taaluma kuwa zaidi ya miaka 60 ambapo uamuzi huu wa Serikali unatokana na wenye taaluma wengi kustaafu huku wakiwa bado na uwezo wa kufanya kazi zaidi.

Waziri mkuu Mizengo Pinda alisema jana suala hilo linapaswa kuangaliwa upya na kwa umakini kufuatia kuwepo na changamoto nyingi za upungufu wa wahadhiri katika vyuo vikuu vingi Tanzania.

Unataka stori kama hizi zisikupite? unataka kuwa kupata kila kinachonifikia? karibu ujiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram Facebook

Tupia Comments