Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Ningependa tu mtambue kuwa nawashkuru na nawapenda sana, na siku zote ntahakikisha najitahidi kadri ya… http://t.co/0SK92pieGq
— Diamond Platnumz (@diamondplatnumz) January 7, 2015
Kata ya Kimara: Tumejenga nyumba ya Mganga wa Zahanati ya Mavurunza kwa Sh 43mil #Utekelezaji #AMUA
— MNYIKA John John (@jjmnyika) January 7, 2015
Kata ya Kimara: Tumejenga wodi ya wanawake ktk Zahanati ya Mavurunza kwa sh 22mil #Utekelezaji — MNYIKA John John (@jjmnyika) January 7, 2015
Nawpenda sana Mashabik wangu ! Kama mtu bado hajaipata nyimbo yangu ya #MALELE atkuwa amekosa uhondo… http://t.co/pY7dWI9FPF
— shilole kiuno (@shilolekiuno) January 6, 2015
Zitto Kabwe:Zinahitajika tshs 500 bilioni kila mwaka kwa miaka 3 mfululizo kuweza kukarabati miundombuni ya Reli Tanzania ( Reli ya ratili 80 ).
Ili kujenga Reli mpya kabisa ya ‘ standard gauge’ zinahitajika $6.5bn
Kwa Nchi kama yetu, bila mtandao wa Reli madhubuti, Uchumi utakua kwa mwendo huu huu wa jongoo badala ya ukuaji wa kasi.
Clouds FM
CHENGE AJIUZULU
WAKATI Watanzania wakisubiri hatima ya Waziri wa Madini na Nishati Profesa Sospeter Muhongo, ambaye Rais Kikwete alisema anamuweka kiporo kutokana na kashfa ya Escrow, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mh Andrew Chenge, ametangaza rasmi kuachia nafasi hiyo.
Bunge lililopita baada ya kujadili ripoti CAG kuhusu miamala ilyofanyika kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania, lilipitisha maazimio manane ikiwemo kuwajibishwa viongozi wa Serikali na wale wa kamati za Bunge walionekana kuhusika katika kashfa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa, Chenge alitangaza kujiuzulu nafasi yake juzi baada ya kamati yake kukutana kwenye ofisi ndogo za Bunge jijijni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya shughuli za Bunge, John Joel, alipotakiwa kuthibitisha hili, alisema hayuko ofisini, hivyo hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja.
RC atoa siku 5 albino apatikane
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo ametoa siku tano kuanzia juzi Jumatatu kwa watendaji, sungusungu na wakazi wa kijiji cha Ndami, tarafa ya Mwambashimba wilayani Kwimba kuhakikisha mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Pendo Emmanuel (4) aliyeporwa na watu wasiojulikana anapatikana akiwa hai ama mwili wake.
Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wakazi wa kijiji hicho na watendaji wa wilaya ya Kwimba ambapo alisema mazingira hayaoneshi kama mlango ulipigwa jiwe kubwa maarufu kama ‘fatuma’.
Alisema Kwimba ina watu 74 wenye ulemavu wa ngozi huku mtoto Pendo jina lake likiwa la tisa, lakini inashangaza kusikia siku ya tukio, Desemba 27 mwaka jana majira ya saa 3 usiku sungusungu wote walikwenda kula na muda mfupi baadaye mtoto huyo aliibwa baada ya kuvamia nyumba aliyokuwamo.
Blogs
Mwananchi: Umeme wa gesi kuanza mwezi ujao
Dar es Salaam. Watanzania waliokuwa wakisubiri kwa hamu kuanza kutumia umeme utokanao na mradi wa gesi asilia wa Kinyerezi, sasa watahitajika kuvuta subira kidogo kutokana na uzalishaji wa nishati hiyo kusogezwa hadi katikati ya mwezi ujao.
Awali, maofisa wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na makandarasi wa mradi kwa nyakati tofauti, walinukuliwa kuwa ujenzi ungekamilika Desemba mwaka jana na uzalishaji wa majaribio ungeanza mapema mwezi huu.
Hata hivyo, ripoti ya maendeleo ya mradi huo iliyotolewa jana na TPDC inaonyesha kuwa baadhi ya masuala ya ujenzi na ununuzi yanatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu na Februari.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ujenzi wa mradi mzima wa bomba hilo la gesi linalotokea Mtwara hadi Kinyerezi, ulikuwa umekamilika kwa asilimia 94.8 wakati ununuzi ulikuwa ni asilimia 99 mwishoni mwa Novemba.
Akielezea kilichochelewesha, Meneja wa mradi huo kutoka TPDC, Kapuulya Musomba alisema kuwa uzalishaji wa majaribio umesogezwa kutokana na tatizo la usafirishaji wa vifaa lililoathiri ratiba ya awali. Uzalishaji rasmi unatarajiwa kuanza Juni mwaka huu.
“Kuna wakati tulikuwa tukitegemea mitambo iliyoingia bandarini ingetolewa ndani ya wiki moja, lakini haikuwa hivyo,” alisema Musomba.
Kuhusu uwapo wa uchakachuaji wa kuongeza bei mara mbili ya mradi huo, Musomba alisema kiasi cha Sh2 trilioni walizoomba kukamilisha ujenzi huo ndizo zilizomo kwenye mkataba. Novemba, 2014 akiwa mjini Nzega, mkoani Tabora, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwatuhumu vigogo wa Serikali kwa ufisadi wa kuongeza Dola 600 milioni za Marekani (Sh1.02 trilioni) katika ujenzi wa mradi huo hali iliyofanya gharama ziongezeke mara mbili na kufikia Sh2.4 trilioni.
Alisema kuwa awali kampuni inayojenga bomba hilo, ilisema gharama halisi za mradi huo ilikuwa Sh1.20 trilioni, lakini wao wakaongeza mara mbili ya fedha hizo kwa manufaa yao binafsi.
BBC Swahili: Alshabaab ladai kuwaua wapelelezi wa USA
Wapiganaji wa kundi la Alshabaab kutoka Somalia wanasema kuwa wamewaua watu wanne wanaodaiwa kuwa wapelelezi wa Marekani,Ethiopia na serikali ya Somalia.
Wanne hao wanadaiwa kupigwa risasi katika mji wa Baradhere siku ya jumanne baada ya jaji mmoja wa Alshabaab kuwapata na hatia ya kuwaunga mkono wapelelezi wa CIA na mashirika yanayokabiliana na kundi hilo.
Wiki iliopita maafisa wa Somali wanasema kuwa shambulizi moja la ndege lililotekelezwa na Marekani lilimuua kiongozi wa ujasusi wa Alshabaab Abdishakur Tahlil.
BBC Swahili:Song astaafu soka ya kimataifa
Mchezaji wa Cameroon West Ham Alex Song amestaafu kucheza soka ya kimataifa baada ya kutopata mwaliko wa kikosi cha timu ya taifa kitakacholiwakilisha taifa hilo katika kombe la nchi za Afrika.
Song mwenye umri wa 27, ambaye kwa sasa anachezea timu ya ligi kuu ya Uingereza West Ham kupitia mkopo wa Barcelona sasa ataweza kuendelea kuichezea West Ham baada ya mazungumzo ya dakika za mwisho na Cameroon kuvunjika.
Song hajaichezea timu yake ya taifa tangu alipopewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Croatia katika ngazi ya makundi katika Kombe la Dunia 2014.
Mwana habari za Michezo Saleh Jembe
INANUKIA, SAFARI YA JOSEPH OWINO KUIAGA SIMBA IMEWADIA
Benchi limetajwa ndiyo chanzo cha beki wa kati wa Simba Mganda, Joseph Owino kuchukua maamuzi ya kurudi kwao na kuiacha timu hiyo inayoendelea na michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Beki huyo, hivi karibuni alirejea nyumbani kwao Uganda mara baada ya kumalizika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar iliyomalizika kwa Simba kufungwa bao 1-0 huku Owino akianzia benchi.
Wakati hali hiyo ikiendelea, zipo tetesi kuwa beki huyo aliyebakisha miezi sita kwenye mkataba wake, amepangwa kuondolewa kwenye usajili wa msimu ujao wa ligi kuu ili nafasi yake ichukuliwe na Mkenya, Paul Kiongera ambaye anaendelea na matibabu.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa beki huyo, Owino hana matatizo yoyote ya kifamilia yaliyomsababishia arejee kwao zaidi kukerwa na kitendo cha yeye kuwekwa benchi.
Chanzo hicho kilisema, beki huyo alianza kushtukia kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa na mechi kumalizika kwa Simba kushinda mabao 2-0 ambayo alianzia benchi lakini baadaye akaingia.
“Ugumu wa namba kwa Owino ulianza baada ya timu hiyo kumsajili Musheed (Juko) katika usajili wa dirisha dogo kwa ajili ya kukiboresha kikosi hicho.
“Wakati anasajiliwa beki huyo, Owino alijua kwamba yeye watacheza pamoja, lakini baadaye mambo yakabadilika na nafasi yake kupangwa Isihaka (Hassani).
“Kwa mujibu wa Owino, yeye alikuwa ameshtukia kuwepo na mipango kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa timu hiyo ambaye yeye hamtaki Owino, hivyo akaona ni vyema aondoke zake ili awapishe mabeki hao waendelee kuichezea Simba,”kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Katibu Mkuu wa timu hiyo, Stephene Ally kuhusiana na beki huyo alisema kuwa: Owino aliomba ruhusu baada ya kumalizika mechi dhidi ya Kagera.”
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook