Habari za Mastaa

Str8uplive kutua nchini Uganda, kupanda jukwaa moja na mkali wa Nigeria ‘Fireboy’

on

Najua Nina watu wangu wanaopenda burudani hususani kupitia muziki wa live sasa nina habari njema ninayotaka kukujuza ni kwamba kuna vijana wenye utashi mkubwa ambao wameungana kwa pamoja ili kuufanya muziki wa bendi kupewa heshima ndani ya nchi hata kimataifa.

Kundi hili linafahamika kama Str8uplive linaundwa na wakali akiwemo Zungu The Drummer, DJ Skadi,Bam Bass, Amo Keys, Mr. Norman, Emmz , Nuri Bedja na pia yakiwemo Taasisi za kibenki.

Miongoni mwa vitu vinavyowashangaza wengi kuhusu wakali hao ni pale wanapokuwa Jukwaani na kisha kuubadilisha wimbo wa msanii kuwa wa tofauti kwa kutumiwa kwa Vyombo vya Muziki.

Mpaka sasa Str8uplive wameziandika rekodi  mbalimbali kwa kufanya kazi na wasanii wakiwemo, Fireboy- Nigeria  , Gyakie – Ghana, Ladipoe – Nigeria , Joe Boy – Nigeria.

Sasa Mwaka 2022 wakali hao wanauanza kwa neema ambapo wanatarajiwa kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya maandalizi yao ya pamoja na mkali Fireboy.

Akizungumza na Millardayo.com Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Str8upvibes alisema..‘Kwanza ningependa kuwashukuru Mashabiki wanaoendelea kutushika mkono hususani waliopo Dar, Moshi, Arusha , Mwanza na mikoani mingine kiukweli ni faraja iliyojaa ndani ya miyoyo yetu’- Sniper Mantana

‘Lengo la kuwepo kwa Str8uplive ni kuupa heshima muziki wa bendi na kuonesha utofauti hususani kwenye muziki wa live bendi na hata nchi yetu kupata heshima’- Sniper Mantana

Aidha Sniper Mantana akasema bendi hiyo inatarajiwa kutoa burudani Mnamo April 30 Nchini Uganda.

“Mbali na kwamba tumeshatoa burudani katika mikoa kadhaa sasa ni muda wetu wa kuwafikia watu wetu wa kimataifa ambapo Str8uplive mwaka huu 2022 Mnamo April 30 wanatarajiwa kutoa burudani ya live bendi nchini Uganda’- Sniper Mantana

‘Kitakachoenda kufanyika nchini Uganda ni kitofauti kidogo kwani Str8uplive wataungana na fireboy jukwaani kwaajili ya kutoa burudani siku ya April 30, 2022 na nina uhakika mashabiki wamejiandaa kuwapokea Str8uplive na hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza bendi hii kutumbuiza katika nchi hiyo‘- Sniper Mantana

‘Na  chakumaliza kusema ningewaomba wadau mbalimbali wa makampuni kama unaona uhitaji wetu wa bendi msisite kuwasiliana nasi kupitia namba 0717671163 kwa maelezo zaidi tuhakikishe tunaendelea kukuza sanaa yetu ili muziki wa bendi upewe kipaumbele zaidi’- Sniper Mantana

Alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Str8upvibes akizungumza kuhusiana na bendi yake iitwayo Struplive inayotarajiwa kutoa burudani nchini Uganda mnamo April 30, 2022 katika tamasha lililoandaliwa na kupewa jina la Fireboy live in Kampala.

WEMA BAADA YA KUMSAIDIA MAMA HUYU KAFUNGUKA “HATA NIKIFA SASA, NTAIONA PEPO”

Soma na hizi

Tupia Comments