Habari za Mastaa

‘Strong Girl remix’ ndani wamo Diamond, Vanessa, D’banj, Waje, Yemi Alade…Video

on

May mwaka huu wasanii mbalimbali wa kike Africa waliungana na kutoa Video ya wimbo wa Strong Girl ikiwa ni kampeni zao za kuhamasisha elimu kwa wanawake na watoto wa kike chini ya nembo yao ya One Campaign.

Mastaa hao wameungana tena na kufanya remix ya wimbo huo ambapo wamewashirikisha wasanii wa kiume kama Waje, D’Banj,Gabriel, Banky W pamoja na Diamond.

Idadi ya wasanii hao kwa sasa walioshiriki katika wimbo huo wa “Strong Girl (Remix)” na nchi wanazotoka ni Waje (Nigeria), D’Banj (Nigeria) Victoria Kimani (Kenya), Vanessa Mdee (Tanzania), Banky W (Nigeria), Arielle T (Gabon),Diamond (Tanzania) Gabriela (Mozambique), Yemi Alade (Nigeria), Selmor Mtukudzi (Zimbabwe), Judith Sephuma (South Africa), Omotola Jalade, Nwafor (South Africa), na U2’s Bono.

Itazame hapa mtu wangu

Video ya awali hii hapa..

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments