Michezo

Suarez afaulu mtihani wa Uraia Italia, njia nyeupe Juventus

on

Staa wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez leo amefanikiwa kufaulu mtihani wa kuomba uraia wa Italia, hivyo sasa anaweza kupata uraia (Passport)

Hatua hiyo imekuja ili Suarez kukwepa vizuizi vya kutaka kujiunga na Juventus mwisho wa msimu, Italia kwa mchezaji anayetoka nje ya umoja wa Ulaya (EU) kuna idadi maalum ya wachezaji inayoruhusiwa kucheza soka katika club moja,

HivyoSuarez anaripotiwa atasaini Juventus mwisho wa msimu kama mchezaji wa raia wa Italia na kukwepa vizuizi hivyo, Suarez anaondoka Barcelona baada ya kutokuwa katika mpango wa kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman.

Soma na hizi

Tupia Comments