Michezo

Suarez kutimkia Atletico Madrid

on

Baada ya kocha wa Juventus ya Italia Andrea Pirlo kunukuliwa akisema kuwa Luis Suarez ni ngumu kuwa mshambuliaji wao sababu ya ishu za uraia wa Italia kuwa ni mchakato mrefu.

Leo imeripotiwa taarifa mpya kuwa nyota huyo wa Uruguay sasa yuko hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kujiunga na club ya Atletico Madrid ya Hispania akitokea FC Barcelona.

Suarez anapambana kutafuta timu ya lwenda kuchezea mapema baada ya kocha wa sasa wa Barcelona Ronald Koeman kuweka bayana kuwa mchezaji huyo hana mipango nae.

VIA : ESPN

Soma na hizi

Tupia Comments