Michezo

Rekodi mpya waliyotengeneza Suarez na Sturridge ndani ya Liverpool

on

1740e8ca149b7a716984d90984ad2291Washambuliaji wa klabu ya Liverpool Daniel Sturridge na Luis Suarez wanazidi kung’ara katika ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Washambuliaji hao wawili ambao ndio vinara wa magoli katika EPL wametengeneza rekodi mpya katika klabu ya Liverpool baada ya mchezo wa jana dhidi ya Sunderland ambao Liverpool walishinda 2-1, Steven Gerrard na Sturridge wakifunga magoli hayo ya ushindi.

Kwa maana hiyo goli la Daniel Sturridge linamaanisha yeye pamoja na Luis Suarez wameweza kufunga 20 na zaidi kila mmoja katika msimu mmoja wa ligi. Hii haijawahi kutokea katika kipindi cha miaka 50 kwa washambuliaji wawili wa Liverpool kufunga mabao 40 au zaidi katika ligi.

Tupia Comments