Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema kupungua Kwa Migogoro ya wakulima na wafugaji nchini hususani Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro imetokana na ushirikiano mzuri wa viongozi kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Taifa.
Sumaye ameyasema hayo alipohudhiria hafla kueleleza mafanikio ya miaka miwili ya Serikali ya Wilaya chini ya Mkuu Wilaya hiyo Judith Nguli.
Sumaye amesema Wilaya ya Mvomero ni moja ya maeneo yaliyokuwa yanakabiliwa na changamoto ya migogoro ya ardhi ikihusisha wakulima na wafugaji kipindi cha nyuma lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti changamoto hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa .
Amesema siri kubwa ya mafanikio hayo ni kuwepo kwa ushirikiano mzuri kwa viongozi kuanzia ngazi ya chini hadi juu pamoja na wananchi.
“tunakila sababu ya kuisifu Serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Mhe. dokta Sami Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira na mipango mizuri kwenye sekta ya kilimo na mifugo ”
Kwa upande wake Mkuu w Wilaya ya Mvomero Judith Nguli amesema tangu kuanzishwa Kwa Kampeni ya Tutunzane Mvomero ambayo ilizinduliwa na Rais Samia Suluhu Hasaan Mwezi Agosti mwaka 2024 imekuwa na mafanikio na sasa wakulima na wafugaji zaidi ya 700 wamejisajili Ili kupata maeneo sahihi ya kupanda malisho na kilimo.
Amesema Kampeni hiyo imewapa hamasa wafugaji na sasa wanaachana ufugaji wa kizamani na Kufuga kisasa ambapo wameanza kupanda malisho ya Mifugo ,kuchimba visima vya kunyweshea maji.
Amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro kwani wafugaji hawatatembeza Mifugo Yao katika mashamba kutafuta malisho na maji.
Naye katibu Chama cha Wafugaji Nchi (CWT) Mathayo Daniel ameomba Serikali kuwlleta Mbegu Bora za ng’ombe Ili wazalishe Mifugo ya kisasa .
Amesema Mbegu hizo zipo nchi za Kenya,Afrika kusini hivyo baadhi ya wafugaji hawataweza kuagiza kutokana na gharama hivyo Serikali iwasaidie kuleta na kuzalisha nchini.
Juma Mlendo mkulima wa Mpunga Mvomero anasema tangu kuanza kwa Kampeni hiyo changamoto imepungua kwani awali walilazimika kulima usiku na mchana mazao Ili yasiliwe na Mifugo.