Mix

Vyakula vitano vinavyoweza kuondoa sumu mwilini kwa wavutaji sigara …

on

Mtu wangu wa nguvu kuna njia nyingi za kuweza kuishi na kujitibu baadhi ya magonjwa kwa vyakula vya asili, hii ni stori ambayo nimekutana nayo kutoka healthypanda.net February 3. Kisayansi huwa inaripotiwa kuwa sigara au uvutaji wa tumbaku unaweza kuleta madhara kwa mtumiaji, kwani tumbaku ina sumu inayojulikana kama Nicotine. Lakini nimekutana nayo list ya vyakula vitano vinavyoweza kuondoa sumu ya Nicotine kwa mujibu wa healthypanda.net.

1- Broccoli inatajwa kuwa na vitamin B5, C na B vitamin ambazo zinatajwa kuwa na kazi kubwa mwilini, ukosefu wa baadhi ya vitamini ina maana kuwa mwili wako utakuwa haufanyi kazi vizuri. Broccoli pia ina gene NRF2 ambazo zinasaidia seli za mapafu kushambuliwa.

2

2- Machungwa – hamu ya uvutaji wa sigara inaweza kumalizwa na uwepo kwa vitamin C kwa wingi katika mwili wako, machungwa ni matunda ambayo yanaweza kusaidia ongezeko la Vitamin C, hivyo inaelezwa kama utafanya hivyo utakuwa umemaliza hamu ya kutaka kuvuta sigara, kitu ambacho kitafanya uepuke kuingiza sumu ya nicotine  mwilini.

Ambersweet_oranges

3- Spinach – inaelezwa kuwa na folic acids au vitamin B9 ambayo intajwa kuwa na uwezo mkubwa kuondoa sumu ya Nicotine mwilini, Nicotine pia inatajwa kusababisha ukosefu wa usingizi kwa watumiaji, hivyo folic acids inaweza kumsaidia mtu kurudi katika hali yake ya kawaida.

Spinach_leaves

4- Malimao– ni moja kati ya silaha muhimu kuweza kupambambana na sumu ya Nicotine muhimu. kwa kawaida inaripotiwa kuwa unapovuta nicotine mwilini inakaa katika mmfumo kwa siku tatu na inaweza haribu seli za ngozi, afya ya ngozi na immunity yaani uwezo wa mwili kupambana na magonjwa, lakini Limao ambalo lina Citric acid na Vitamin C kwa haraka inaweza kusaidia kuondoa vitu visivyohitajika mwilini.

Lemon

5- Carrots – uwepo wa Vitamin A na C katika vyakula vyako vya siku vinaweza kusaidia uondoaji wa sumu ya Nicotine kwa mvutaji wa sigara. Carrot ambayo ina vitamin A, C na K inaimarisha asili ya kinga za mwili.

Carrots

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments