Michezo

Sven awapeleka Simba SC FIFA

on

Imeripotiwa kuwa Kocha wa zamani wa Simba SC Sven Vanderbroeck amaishitaki Club ya Simba SC FIFA kwa kutolipwa madeni yake.

Sven anadai kuwa bado hajalipwa kiasi cha USD 44,000 (Tsh milioni 102) ambazo ni malipo yake ya bonasi ambazo bado hajapatiwa hadi sasa.

Kocha Sven Vanderbroeck aliondoka Simba SC kwa kuvunja mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote mbili miezi mitatu iliyopita na kwenda kujiunga na Club ya FAR Rabat ya Morocco.

Soma na hizi

Tupia Comments