Michezo

Sven sasa Simba SC ni ushindi kila game

on

Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea kwa Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Simba SC walikiwa wageni wa KMC katika uwanja wa Uhuru.

Simba wakifanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli yakiwekwa wavuni na Deo Kanda dakika ya 46 na Gerson Fraga aliyefunga goli la pili dakika za nyongeza kabla ya game kumalizika.

Huu ni ushindi wa tatu wa Simba SC ikiwa chini ya kocha wao mpya raia wa Unelgiji Sven Vanderbroeck, hivyo kocha huyo anaendelea na rekodi ya kutopoteza na kuihakikishia Simba SC kuendelea kuwa kileleni katika mbio za kutetea taji lake.

Soma na hizi

Tupia Comments