Michezo

Ole Gunnar Solskjaer anazidi kuwakatisha tamaa Real Madrid

on

Baada ya kuanza msimu vibaya huku timu yao ya Real Madrid ikiyumba, inaelezwa kuwa uongozi wa Real Madrid bado haujakata tamaa ya kupambania saini ya kiungo wa Man United Paul Pogba, Real Madrid inaamini ina nafasi ya kunasa saini ya staa huyo mwezi January wakati kocha wa Man United Solkjaer bado yupo kwenye mipango yake.

Kama ambavyo Ole Gunnar Solskjaer anamuweka katika mipnago yake, huo unaweza ukawa ugumu zaidi kwa club ya Real Madrid kunasa saini ya staa huyo, kuonesha kuwa Solskjaer hayupo tayari kumuachia Pogba aende kirahisi ameweka wazi kuwa mchezaji huyo haendi popote na hatishiki na tetesi zinazoendelea kwa sasa.

“Sihofii chochote kwa sasa na sitahofia chochote kuhusiana na suala la Pogba kubakia hapa, simsiklizi Rais wa Real Madrid (Perez), kama tuliweza kuishi na hizi tetesi tena, basi tutaweza kuzimudu kama tulivyofanya wakati wa dirisha la usajili la majira ya joto”>>>Ole Gunnar Solskjaer

VIDEO: Moja kati ya magoli ya marehemu Jeba, hili liliwaumiza wana-Simba 2016

Soma na hizi

Tupia Comments