Top Stories

T-shirt za Kilimanjaro dukani Marekani, moja ni zaidi ya Tsh. 50000.

on

Kampuni maarufu ya mavazi ya The North Face ya Marekani imeziingiza sokoni T-shirt zenye jina la Mlima Kilimanjaro uliopo Tanzania na kuuza kila T-shirt moja dola za kimarekani 25 ambazo ni sawa na shilingi elfu hamsini na saba na mia tatu sitini na mbili Tsh.
Maelezo kwenye t-shirt hizo yanaonesha zinatengenezwa El Salvador ambapo kwa mbele zina maandishi machache madogo upande wa kushoto yakiwa yameambatana na nembo ya kampuni hiyo, yanasomeka… Kilimanjaro, The Highest Mountain Peak in Africa.

Upande wa nyuma kuna mchoro mkubwa wa Mlima Kilimanjaro ambao umeambatana na maneno The North Face of Kilimanjaro kwa upande wa juu na chini imeandikwa Tanzania, 19.341 feet 5,895 meters.

EXCLUSIVE: MAISHA YA KAREN, MTOTO WA GARDNER, ALIVYOISHI NA LADY JAY DEE NA KITU ALIMWAMBIA KUHUSU MUZIKI WAKE

FULL INTERVIEW: MTOTO GUMZO ANTHONY KAONGEA TUSIYOYAJUA BAADA YA KUMPELEKA BABA YAKE POLISI

VIDEO: MUME KAENDA KAZINI, WIFE KALETA MCHEPUKO NYUMBANI… 

Soma na hizi

Tupia Comments