Ubunifu ndio unaiendesha dunia lakini sio kila mtu amepewa uwezo wa ubunifu lakini kuna wachache ambao tafiti zinaonyesha kwamba wao ndio wanaongoza kwa akili za ubunifu na ndio maana nimekuletea orodha hii ya nchi 10 zenye ubunifu duniani huku Switzerland ikiongoza orodha hiyo kwa mwaka wa 7 mfululizo.
Top 10 ya nchi za kibunifu zaidi Duniani
- Switzerland
Nchi hii imekuwa ni ya kwanza tangu mwaka 2011 kwa sababu ya uwezo wake wa kubadili mawazo ya kibunifu na kuwa miradi mikubwa yenye faida
2. Israel
Israel ni nchi ambayo inatoa visa maalum kwa Wajasiriamali pia inaongoza kwa uanzilishi wa mbinu za kiusalama mitandaoni pia wanaotarajiwa kuwa wajasiriamali wanapewa mafunzo na jeshi la Israel.
3. Finland – Finland imepewa nafasi kwa sababu ya upatikanaji bora wa Wanasayansi na Wahandisi na kiwango cha juu cha ushirikiano kati ya vyuo vikuu na sekta mbalimbali.
4. Marekani – Marekani inaweza ikawa ndiyo bora kwa kugeuza mawazo ya Chuo kikuu na kuyafanya kuwa ya kibiashara na yenye mafanikio kwa mfano Facebook na Snapchat.
5. Ujerumani ni nchi ambayo imesisitiza zaidi kwenye ubunifu na kuupa nafasi.
6. Sweden
7. Uholanzi – Uholanzi imepata alama za juu za ubora wa taasisi zake za utafiti wa kisayansi na ukaribu wa uhusiano kati ya vyuo vikuu na sekta binafsi.
8. Japan- Ubora wa taasisi za utafiti pamoja na upatikanaji wa Wanasayansi bora na wahandisi kunachangia kwa ujumla mazingira ya nchi hii kuwa ya kibunifu.
9. Singapore
10. Denmark – ni nchi ambayo imeongoza kwa teknolojia ya nishati mbadala ambapo 140% ya mahitaji ya nishati ya nchi hii ni nishati inayotokana na upepo.
ULIPITWA? Tazama hapa chini kuona Wanajeshi Makomando wa Tanzania walivyoonyesha uwezo wao mbele ya Rais Magufuli…. Bonyeza play hapa chini kutazama