Alhamisi ya January 19 2017 michuano ya mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 maarufu kama AFCON ilichezwa katika uwanja wa Franceville nchini Gabon, uwanja wa Franceville unatumiwa kwa michezo ya Kundi B lenye timu za Algeria, Tunisia, Senegal na Zimbabwe.
Mchezo wa kwanza kwa leo umezikutanisha timu za Tunisia dhidi ya Algeria maarufu kama Mbweha wa Jangwani, Algeria ambao wameshuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya sare ya 2-2 dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wao wa kwanza, wamekutana na kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa wapinzani wao Tunisia.
Mchezo kati ya Algeria na Tunisia haukuwa mwepesi na ililazimika kusubiri hadi dakika ya 50 ili kuona nyavu zikicheza, baada ya Ramy Bansebaini kuipatia goli la kwanza Tunisia kabla ya dakika ya 66 Naimi Sliti kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penati, mabadiliko ya kutolewa Yassin Ibrahim dakika ya 74 na kuingia Sofiane Hanni yalizaa matunda kiasi baada ya Hanni kufanikiwa kufunga goli la kufutia machozi dakika ya 90 kwa Algeria.
https://youtu.be/MwBsp4PJmnc
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4