Michezo

UEFA Champions League timu zinaendelea kuushangaza ulimwengu wa soka

on

UEFA Champions League usiku wa April 17 2019 ulikuwa wa kusisimua zaidi katika michezo ya raobo fainali ya mwisho, game ya Man City dhidi ya Tottenham ndio ilikuwa game ya kusisimua zaidi kutokana na mvuto na presha ya mechi hiyo ilivyokuwa kwa pande zote mbili.

Hadi dakika 90 zinamalizika mchezo ulikuwa na mvuto na hamasa kubwa kutokana na magoli mengi kufungwa, game hiyo ilimalizika kwa Man City kupata ushindi wa magoli 4-3 lakini aggregate ikawa 4-4 ila Man City ameruhusu magoli mengi nyumbani.

Matokeo hayo sasa yanawafanya Tottenham kuingia hatua ya nusu fainali na watacheza dhidi ya Ajax wakati Liverpool ambao wamewatoa FC Porto 4-1 (Aggregate 6-1) watacheza dhidi ya FC Barcelona ya Hispania, game hizo zinatajwa kuwa zitakuwa za kuvutia kutokana na timu zote hizo kuwa na kiwango bora hususani, game ya Ajax na Tottenham inatajwa kuwa itakuwa ngumu.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments