Top Stories

MSAMI KAFUNGUKA “Sikuwa na mpango na Wanawake niliokua nao”

on

Ayo TV na millardayo.com zinaye Msami kwenye EXCLUSIVE na kaeleza mambo mengi lakini kubwa ni kuhusu kuwa kwenye mahusiano na baadhi ya mastaa wenzake ambao wengi hawakufahamu hadi pale alipoamua kufunguka.

>>>”Kwanza labda tuifanye hii iwe mara ya mwisho na leo naweza kuzungumza labda watu hawakuwahi kufahamu na mimi sijawahi kuzungumzia mambo ya mahusiano yangu. Sio mbaya watu wakizungumza kuhusu mimi juu ya uhusiano wangu.

Wasanii wengi ambao wapo kwenye mahusiano wanakuwa kama wanaigiza mahusiano. Mimi nikiwa kwenye mahusiano na staa wa Bongo Movie basi natofautisha kati ya maisha yangu niliyokuwa nikiisha na uhusiano wangu.

Irene Uwoya nilimtambulisha kwa ndugu zangu mpaka famili yake inanijua, pia familia yangu inamjua na sijawahi kufikiria kwamba kuna lolote litakuja kutokea. Tulikuwa hatupendelei mambo ya mitandao ya kijamii. Kimsingi nimejifunza mengi mtu akiwa na uhusiano na watu maarufu. Ningependa kutoa somo kwa wengi wasipende.

“Ni kweli nilikuwa na date na Irene Uwoya. Tumekaa takribani miaka miwili wengi walikuwa hawafahamu hilo na kuna kipindi tulikuwa kwenye mahusiano na tukaachana. Kwa hiyo, ni mtu ambae alikuwa ananipenda na mimi nampenda sana ila kuna vitu vilitokea ambavyo sio vizuri.” – Msami.

“Hakuna aliyelipwa wala Ben Pol hajanilipa” – Ebitoke kwenye Ala za Roho…play kwenye video hii kutazama!!!

Soma na hizi

Tupia Comments