Michezo

Hazard kawapiga mbili West Ham, waandishi wakamuuliza ni kweli anahamia Real Madrid?

on

Club ya Chelsea usiku wa April 8 2019 ilicheza game yake ya 33 ya Ligi Kuu England dhidi ya West Ham United, huo ukiwa ni muendelezo wa harakati zao za kuwania kumaliza TOP 4 katika Ligi Kuu ya England ili wakate tiketi ya kucheza UEFA Champions League kwa msimu ujao wa 2019/2020.

Chelsea wakiwa nyumbani wamefanikiwa kuingia TOP 4 wakati huu wakilazimika kusubiri matokeo ya game za Tottenham na Arsenal, Chelsea wamefanikiwa kupata ushindi wa mgaoli    2-0, magoli yakitiwa nyavuni na staa wao Eden Hazard aliyefunga yote mawili dakika ya 24 na 90 ya mchezo huo.

Baada ya game kumalizika wakati wa mahojiano Eden Hazard aliulizwa kuhusiana na tetesi za kwenda Real Madrid mwisho wa msimu na alijibu hivi “Kwa sasa naiangalia Chelsea hadi mwisho wa msimu, nataka tumalize TOP 4 na Europa League bado tuna mengi ya kufanya halafu tutaona”>>>Hazard

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments