Michezo

Arsenal wanahitaji majibu kutoka UEFA fainali ya Europa League kupelekwa Baku

on

Club ya Arsenal ya England bado inahitaji majibu kutoka kwa chama cha soka Ulaya UEFA kuhusiana na uamuzi wao wa kuipeleka fainali ya UEFA Europa League Ulaya Mashariki (Baku), sehemu ambayo ni ngumu kwa mashabiki wa timu za Arsenal na Chelsea ambazo zimefuzu kucheza fainali ni ngumu kufika kutokea London.

Arsenal na Chelsea watacheza mchezo wa fainali ya Europa League May 29 2019 katika mji Baku nchini Azerbaijan, Arsenal wameeleza kusikitishwa na sehemu utakapochezewa mchezo huo, kwani inakuwa ni changamoto kubwa kwao kupata mashabiki wao wanatokeo London.

Pamoja na awali vilabu vya Chelsea na Arsenal kulalamikia kuwa wamepewa idadi ndogo ya tiketi 6000 kila mmoja za mashabiki wao, inaelezwa kuwa safari ya kwenda Baku inaweza kuwagharimu saa 50 kwa njia ya ardhini, huu ni umbali mrefu zaidi kwa mashabiki wao kwenda kuhudhuria na uliwahi kuzungumzia na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments