Mix

Wema Sepetu kalamba ubalozi na kuzindua ST Kids

on

Msanii wa filamu Tanzania Wema Sepetu leo ametangaza kuwa balozi wa kampuni ya Star Times sambamba na kuambana na uzinduzi wa chaneli mpya ya katuni ya watoto, chaneli ambayo itakuwa inalenga kuburudisha na kuelemisha watoto.

Wema Sepetu akiwa pamoja na Dina Marios wameambatana kwa pamoja na uongozi wa Star Times kuzindua chaneli ya kwanza ya katuni Tanzania Star Times Kids itakayokuwa katuni zake zinatumia lugha ya Kiswahili ili kuendena na walengwa hasa wa chaneli hiyo ambayo ni watoto wa kitanzania wanaozungumza na kusikia lugha ya Kiswahili kwa kiwango kikubwa.

ST Kids ni mahususi kwa ajili ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 5 hadi 9, maudhui yake yanalenga kuwajengea watoto uwezo wa kuwa wabunifu na kuhusiana vizuri na wazazi wao, hii ni chaneli ya kwanza ya watoto Tanzania ambayo vipindi vyake vitakuwa katika lugha ya Kiswahili hivyo ni nafasi ya kipekee kwa wazazi kuwapatia watoto wao kilicho bora kwa ajili ya ukuaji bora.

Katuni ambazo zitakuwa katika lugha ya Kiswahili ni pamoja na Bonnie Bears, Jingju Cat (Paka wa Opera), Forest Frenzy of Bonnie Bear na Foolish Wolf and his Friends. Vipindi vitaanza kuoneka saa 12 jioni hadi saa 2 Usiku na vitakuwa vikiwa vikurudiwa kwa nyakati tofauti, pia kutakuwa na vipindi vingine vitakavyokuwa vikifundisha watoto kama michezo, kuchora, kutengeneza maumbo na nyimbo.

Kauli ya Bodi ya Filamu kwa waigizaji “Wathaminiwe kama wafanyakazi,nidhamu ya fedha” (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments