Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Innocent Bashungwa amethibitisha taarifa za kifo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga aitwae Fatuma Omari Latu pamoja na Dereva wake aitwae Alex, vilivyotokea kwa ajali ya gari leo mchana wakitokea mkoani Mbeya kwenye Mkutano wa ALAT na kwamba hakuna Mkuu wa Wilaya aliyefariki kwenye ajali hiyo kama ilivyoripotiwa hapo awali.
Hapa unaweza ukabonyeza play kusikiliza alichozungumza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera kuhusiana na ajali hiyo.