Michezo

Danny Rose kamchana Ruud Gullit “atakula maneno yake sasa”

on

Beki wa Tottenham Hotspurs Danny Rose amemjia juu  kiungo wa zamani wa Chelsea Ruud Gullit baada ya awali kueleza kuwa Tottenham watapoteza mchezo wa marudiano dhidi ya Ajax na kutolewa katika michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 , kutokana na wachezaji wa Tottenhamna Danny Rose mwenye kutokuwa na mbinu.

Ruud Gullit ambaye pia ni mchambuzi wa  alinukuliwa baada ya mchezo wa kwanza Tottenham kupoteza kwa goli 1-0, kuwa Dele Alli, Victor Wanyama na Danny Rose pia hawako vizuri, hivyo hashangai na kuona hawafanyi vizuri, Danny Rose leo kaibuka na kusema kuwa Ruud Gullit atakula maneno yake Tottenham Hotspurs imeishangaza dunia.

Ruud Gullit

Tottenham licha ya kufungwa 1-0 nyumbani kwao walienda Uholanzi kupindua matokeo na kujikuta wakishinda 3-2, hiyo ni baada ya Ajax kuanza kuongoza 2-0 hadi kipindi cha pili hivyo mchezo ulimalizika kwa aggregate ya 3-3 lakini Tottenham wakafuzu kwa goli la ugenini kutokana na Ajax wameruhusu kufungwa magoli mengi nyumbani.

“Unajua kuona watu wanaongea kama Ruud Gullit baada ya mchezo wa kwanza na kwa namna alivyokuwa na dharau, vizuri ndio maana tulipambana usiku ule kumnyamazisha, alikuwa amelenga mchezaji mmoja mmoja dhidi yetu na kueleza kwa namna gani tulivyokuwa wabaya, kumbe yale yalikuwa ni mafuta tu katika moto naimani anakula maneno yake”>>> Danny Rose

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments