Michezo

Kuanzia Yanga, Kelvin Yondani hadi Aggrey Morris wa Azam FC wamepigwa faini na kufungiwa

on

Kutoka shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetangaza kuwafungia wachezaji mbalimbali wa vilabu vya Ligi Kuu Tanzania bara, TFF imetangaza kuwaadhibu nahodha wa Azam FC Aggrey Moris na beki wa Yanga Kelvin Yondani.

Kelvin Yondani wa Yanga amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Tsh. 500,000, baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar FC katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 11, 2019 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Aggrey Morris wa Azam FC amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Tsh 500,000, baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Mbao FC katika mechi hiyo ya Aprili7, 2019 iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, hata hivyo Yanga nao wamepigwa faini ya Tsh. 500,000 kutokana na washabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi wakati wakirejea vyumbani baada ya mechi hiyo kumalizika.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments