Michezo

Hii ndio adhabu aliyopewa Diego Costa kwa kumtukana muamuzi

on

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa amerudi tena kwenye headlines baada ya kukutana na adhabu ya kufungiwa, Diego Costa leo imetangazwa amefungiwa kucheza mechi 8 baada ya kuthibitika kuwa Costa alimtukana refa Jesus Gil.

Costa amefungiwa kucheza mechi 8 za Ligi Kuu Hispania maarufu kwa jina la LaLiga kwa kumtusi mama mzazi wa refa, kosa hilo alilitenda Diego Costa wakati wa mchezo dhidi ya FC Barcelona katika uwanja wa Nou Camp ambao ulichezeshwa na refa Jesus Gil hivyo baada ya kushindwa kukubaliana na muamuzi hiyo ndio akatoa lugha hiyo.

Tukio hilo lilitokea April 6 2019 katika mchezo huo wa LaLiga ambao Atletico alipoteza, Diego Costa alilalamika akiwa anaamini kuwa alichezewa faulo ila kutokana na kutoa lugha yake ya matusi akajikuta kaoneshwa kadi nyekundu dakika ya 28 na kutolewa nje, kwa maana hiyo Costa msimu wake wa LaLiga ndio umeisha hivyo akiiacha timu yake ya Atletico ikiwa na mechi 7.

Rais Karia kaiomba kamati ya RC Paul Makonda kuhamishia nguvu kwa Serengeti Boys

Soma na hizi

Tupia Comments