Mix

RC Makonda aendeleza faraja kwa waandishi wa habari

on

leo January 5, 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ameahidi Kuijengea Nyumba Familia ya Mwandishi wa Magazeti ya Serikali TSN wanaochapisha Magazeti ya Habari Leo na Daily News Marehemu Athumani Hamis ambae amezikwa Leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Ahadi hiyo Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TSN, Dr. Yonaz kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambae aliombwa kuisadia familia ya Marehemu ambayo ina watoto Wanne wanaosoma huku wakiwa wanaishi kwenye Nyumba ya kupanga kutokana na Baba yao kuugua kwa zaidi ya Miaka 10 na hivyo kushindwa kufanya kazi.

Dr. Yonaz amesema Makonda kwa kutambua mchango wa tasnia ya Habari hususani waandishi wa Habari amekubali kujenga Nyumba hiyo kama kielelezo cha Kumuenzi Marehemu Athumani ambae katika Uhai wake alikuwa Mpiga Picha na  Mahiri wa Magazeti ya Serikali nchini.

ULIIKOSA HII YA MAKONDA KUMJIBU WEMA BASI BONYEZA PLAY UFAHAMU YOTE

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments