AyoTV

VIDEO: Man Fongo kaeleza tofauti zake na Mensen Selekta

on

Zimepita wiki kadhaa tangu tusikie tofauti za Man Fongo na producer Mensen Selekta, sasa leo April 28, 2017 Man Fongo amekaa na millardayo.com & Ayo TV kaeleza kilichopeleka wawili hao kutoelewana.

Mensen Selekta aliongea na uongozi wangu kwamba kuna kazi imetokea lakini sikuambiwa chochote bali aliniambia anahitaji kitambulisho changu akaniambia niende nyumbani nirudi Studio Jumatatu basi kumbe kulikuwa na dili la tangazo ambalo hiyo siku niliyomletea kitambulisho ndio alikuwa anaenda kuchukua pesa’- Man Fongo

‘Mara ilipofika hiyo siku nikapigiwa simu kama kawaida nikaenda Studio mara naambiwa kuna kazi ya tangazo wakati uongozi wangu ulikuwa bado haujafahamu hiyo pesa na kiasi tunachoingiza kuuliza nikaambiwa imetoka milioni 3 mara mimi nitachukua laki mbili na itakayobaki Mensen Selekta kasema atarekebisha Studio basi baada ya kutoka pale studio nikakutana na baadhi ya wasanii wenzangu nikaambiwa amechukua zaidi ya milioni 3’- Man Fongo

Unaweza kumtazama Man Fongo akielezea tofauti zake na Mensen Selekta

ULIIKOSA HII YA AT KUZUNGUMZIA KINACHOENDELEA KATI YAKE NA MSAMI

Tupia Comments